Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kisiasa na Vyombo vya Habari cha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Lebanon amesema kuwa ‘Operesheni ya ‘Kimbunga cha Al-Aqsa’ ilibadilisha milinganyo yote ya awali ya kisiasa na kijeshi, huku akisisitiza kuwa istiqama na mapambano ya taifa la Palestina vinapaswa kuenziwa kwa siku 1,000 baada ya kuanza operesheni hiyo kubwa dhidi ya Israel.

“Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa’, iliyonza tarehe 7 Oktoba 2023ilikuwa hatua muhimu ya mabadiliko katika mwenendo wa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoikalia Palestina kwa mabavu; kwa kuwa ilidhihirisha ilionyesha uwezo wa makundi ya muqawama ya Palestina ya kufanya ubunifu na kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja za kisiasa na kijeshi,” ameeleza Abdel Majid al-Awad jana Jumamosi.

Amesisitiza kuwa, operesheni hiyo ilisambaratisha na kuvunja ile fikra ya kutoshindwa Tel Aviv na kuondoa taswira ya uwongo kwamba jeshi la Israel ni salama na bora; taswira ambayo viongozi wa utawala huo haramu wamekuwa wakiidhihirisha kwa miongo kadhaa.

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kisiasa na Vyombo vya Habari cha Harakati ya Hamas ya Palestina nchini Lebanon amesema: Wakati wav ta; Ukanda waGaza ulikuwa shabaha ya mashambulizi ya kikatili ya Isrtael yaliyoathiri njanja zote za maisha na kuambatana na mauaji ya kimbari, uharibifu mkubwana kushtadi maafa ya binadamu.

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Hamas amesema kuwa utawala wa Tel Aviv uliainisha malengo kadhaa kwa ajili ya mashambulizi ya umwagaji damu dhidi ya Gaza ikiwa ni pamoja na kuyatokomeza makundi ya muqawama n.k, hata hivyo haukuweza kutimiza malengo yake hayo licha ya kupita muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *