KIUNGO wa zwa  Singida Black Stars, Khalid Aucho, baada ya kumaliza mkataba wake, imeelezwa amepata ofa kutoka timu mbili za Kenya.

Mwanaspoti lilipata taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Aucho kwamba, timu zilizotuma ofa za kuhitaji huduma yake ni Kenya Police FC na AFC Leopards SC zinazoshiriki Ligi Kuu ya Kenya. Pia kuna timu moja kutoka Uarabuni nayo inamuhitaji.

“Bado hajafanya uamuzi kama atasaini Kenya ama timu ambayo inamtaka ya Uarabuni,” alisema mtu wa karibuni na staa huyo.

Alisema, mbali na timu hizo, pia Singida imempa ofa ya mkataba mwingine, hata hivyo hakuonyesha utayari wa kuendelea kusalia na timu hiyo aliyojiunga nayo mwanzoni mwa msimu wa 2025-2026 akitokea Yanga alipomaliza mkataba wake.

“Ingawa siwezi kusema moja kwa moja kwamba hatasaini kabisa Singida, wakati mwingine pesa zinaongea na zina nguvu, ila hadi sasa ni timu hizo ambazo zinahitaji ofa yake,” alisema mtu huyo.

Aucho kwa mara ya kwanza kucheza hapa nchini alijiunga na klabu ya Yanga msimu wa 2021-2022, akaitumikia timu hiyo hadi 2024-2025 ambapo aliisaidia kunyakua mataji manne ya Ligi Kuu, kisha alipojiunga na Singida msimu wa 2025-2026 alichukua ubingwa wa CECAFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *