Donald Trump, Rais wa Marekani amesema muda wa usitishaji vita na Iran umekamilika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli yake imejiri baada ya nchi yake kuishambulia Iran usiku wa kuamkia leo Jumatano, Tehran nayo ikiripoti kulenga kambi za wanajeshi wa Marekani katika nchi za Ghuba.

Baada ya tangazo la Trump kuhusu kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Tehran na Washington, bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa imepanda kwa asilimia tano.

Akizungumza katika mkutano wa nchi za NATO jijini Ankara, Rais Trump amesema hataki tena kushirkiana na Iran

“Makubaliano yamevunjika. Kufanya nao kazi ni kupoteza muda tu.” Amesema Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *