Wachezaji wa Yanga, Dickson Job, Kibwana Shomary na Abuutwalib Mshery wametoa msaada wa madawati 200, madaftari 3000, mabegi katika shule ya Msingi Kilonga.

Msaada huo umekabidhiwa leo katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya huduma za kijamii zinazofanywa na wachezaji hao kupitia Tamasha lao la Wape Tabasamu.

Kilele cha Tamasha hilo kinatarajiwa kufanyika Jumamosi kwa mechi ya kirafiki inayokutanisha nyota wa timu za Ligi Kuu ambao wataunda timu mbili.

Mkuu wa Wilaya Morogoro, Mussa Kilakala amewapongeza wachezaji hao na kuwaomba wakazi wa Morogoro wawaunge mkono.

“Mmefanya kazi kubwa sana kwa kuendelea kuwapa

tabasamu wanafunzi , leo tumepokea madawati 200 , uniform, mabegi na madaftari kwa wanafunzi kwenye hilo tunawashukuru sana.

“Mlikuwa mnaweza kuzisaidia familia zenu lakini

mkasema hapana mje kuipa tabasamu Morogoro , kwenye hili tunawaombea mfanye vizuri mkiwa uwanjani.

“Nawaomba sana watu wa Morogoro siku ya

Jumamosi tujitokeze kwa wingi sana uwanja wa

Jamhuri , hadi kufika saa 9 mageti yawe yamefungwa uwanja umejaa,” amesema Kilakala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *