Rais Samia Suluhu Hassan, amewaonya wanaojiita wanaharakati kwa jina ili kutambulika duniani, lakini kiuhalisia matendo yao ni ya kigaidi, yanayohusisha uvunjifu wa amani, uharibifu wa mali na miundombinu.

Pia, amesema ugaidi ni vitendo vinavyokusudia kuitishia jamii au kuishurutisha Serikali ikubaliane na matakwa ya watu au kundi fulani kwa ajili ya kutimiza haja za kisiasa, kiitikadi au kidini.

Rais Samia ameyasema hayo visiwani Zanzibar leo, Alhamisi Julai 9, 2026 alipohutubia wakati wa hafla ya utiaji saini Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar.

Mkuu huyo wa nchi, amesema kwa mustabali wa dunia ya sasa, ugaidi unaweza kufanyika pia kwa lengo la kuirudisha nyuma nchi inayoendelea kwa kasi.

“Watu au kundi hilo, linakuwa na kauli zinazovaa sura ya kizalendo lakini kwa undani ni maslahi binafsi. Mtu anayependa nchi yake kiukweli huijenga na sio kuibomoa,” amesema.

Amesema vitendo vya kigaidi havikubaliki duniani kote na kila nchi inatumia nguvu ya dola kuhami raia na heshima yake, hivyo Tanzania haitasita kufanya hivyo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *