Wakati huu raia wa Sudan Kusini wakiadhimisha miaka 15 tangu kujipatia uhuru kutoka kwa Sudan mwaka wa 2011, matumaini yao yanaendelea kufifia, suala la amani ya kudumu likiwa bado ni changamoto.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka mingi ya kupigania uhuru, Juba ilitumbukia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka wa 2013 na 2018, vita ambavyo inaelezwa kuwa vilisababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya raia wake.

Licha ya kwamba mwaka 2018 kuliafikiwa mkataba wa amani wa kusitisha vita, mashirika ya misaada yanasema utekelezwaji wake umekwama.

Raia wengi wa Sudan Kusini wamekuwa wakihoji ni lini makubaliano hayo yatatekelezwa kikamilifu ili wapate matunda ya uhuru wao.

Hadi kufikia sasa, Sudan Kusini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mapigano ya kikabila, vurugu za wizi wa mifugo na hata mauaji mengine yanayotekelezwa na makundi yenye silaha.

Aidha ufisadi, ukabila na taasisi zilizodhoofika imetajwa kuwa kizingiti kwa mchakato wa maridhiano ya kitaifa na umoja.

Mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, wafanyakazi wa umaa kukosa kulipwa mishara, elimu duni, mifumo mibovu ya afya na kutopatikana kwa maji safi bado ni changamoto kwa raia wa Sudan Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *