Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Human Rights Watch, limelaani kile inachosema ni ukandamizaji unaofanywa na mamlaka nchini Tunisia dhidi ya wapinzani wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika hili linaungana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya asasi za kiraia katika kuelezea wasiwasi wake kuhusu mgogoro wa haki za binadamu unaozidi kuongezeka nchini humo.

Miaka mitano baada ya Rais Kais Saied, kuchukua madaraka na kujiongezea mamlaka zaidi ya kiutendaji, Human Rights Watch inasema hali ya haki za binadamu imezorota sana.

Human Rights Watch inasema udikteta ulioibuka upya umesababisha ukandamizaji wa mfumo wa asasi za kiraia, waandishi wa habari, wapinzani wa kisiasa, wanasheria huru, wahamiaji na kuvunjika kwa utawala wa sheria.

Viongozi wa shirika hili wakizungumza katika kikao cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, wametoa wito kwa baraza hilo na nchi wanachama kuvunja ukimya na kulaani ukandamizaji huo hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *