Baadhi ya waandamanaji nchini Afrika Kusini wanaopinga uwepo wa wageni wasio na vibali nchini humo, Alhamisi Julai 2026 walipita nyumba kwa nyumba kwenye baadhi ya vitongoji vya jiji la Johannesburg kuwakamata wageni na kuwakabidhi kwa polisi, kitendo kilishozidisha hofu kwa jamii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya hapo jana yamefanyika siku chache kupita tangu kushuhudiwa kwa maandamano makubwa zaidi ya Juni 30, tarehe ya mwisho ambayo haikuwa rasmi iliyotolewa kwa wageni wasio na vibali kuondoka nchini humo.

Katika kitongoji cha Alexandria, jijini Johannesburg kulishuhudiwa waandamanaji wakiingia nyumba kwa nyumba na wakati mwingine wakivunja milango na madirisha kuwatoa kwa nguvu watu inaoamini hawana vibali.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa kwenye eneo la Soweto, ambako waandamanaji waliobeba zana za jadi na bendera walionekana wakikagua nyumba za wenyeji.

Vitendo hivi vya rais kujichukulia sheria mkononi kwa kuvamia na kuwakamata kwa nguvu wageni ambao baadhi wana vibali, vinafanyika licha ya onyo lililotolewa na rais Cyril Ramaphosa, ambaye aliahidi kuwachukulia hatua raia watakaofanya majukumu ya idara ya uhamiaji.

Maandamano dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini, yamesababisha mvutano wa kidiplomasia na baadhi ya mataifa ya Afrika ambayo raia wake wamefukuzwa kwa nguvu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *