
Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayyid Aali Khamenei amezikwa katika Haram ya Imam Ridha (a.s) mjini Mash’had kaskazini mashariki mwa Iran.
Hayati Imam Khamenei amezikwa katika Ukumbi wa Dar al-Dhikr ndani ya Haram Takatifu ya Imam Ridha (a.s).
Maziko hayo yalifanyika baada ya hatua ya mwisho ya kuuaga mwili wake hapo jana shughuli iliyohuudhuriwa na mamilioni ya watuu katika mji wa Mash’had.
Wakiwa na nyuso za huzuni, ghamu na masikitiko makubwa, waombolezaji hao wakiwa wamevaa mavazi meusi kama ishara ya simanzi kwa tukio chungu la kuondokewa na kiongozi wao walibubujikwa na machozi na kuangua vilio.
Mazishi ya jana yalihudhuriwa na raia wa kawaida, viongozi wa kisiasa kutoka zaidi ya nchi 45 duniani ambao wamejitokea leo katika mji huo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huuyo shupavu aliyeuawa kidhulma Februari 28 mwaka huu kufuatia mashambulio ya kijeshi ya Marekani na utawala haramu wa Israel katika mji wa Tehran.
Aidha maombolezo hayo yamehudhuriwa na wanazuoni wa Kiislamu, viongozi wa dini mbalimbali na wasomi kutoka zaidi ya nchi 90 duniani.
Kushiriki mamilioni ya watu katika mazishi haya kunatoa ujumbe muhimu sana. Mojawapo ya jumbe muhimu zaidi ni imani thabiti ya wananchi wa Iran kwamba kiongozi huyo aliyeuawa shahidi alijitolea maisha yake yote kwa ajili ya kulinda Uislamu, Mapinduzi na heshima ya Iran ya Kiislamu. Mahudhurio haya makubwa ya umma ni ishara ya shukrani kwa juhudi zisizo na kikomo zilizofanywa na kiongozi huyo kwa ajili ya Uislamu na Iran, juhudi alizozidhamini kwa maisha yake mwenyewe na ya wanafamilia wake. Ujumbe mwingine muhimu uliotolewa na mahudhurio ya mamilioni ya watu katika msafara wa mazishi ya kiongozi huyo adhimu wa Mapinduzi ni sisitizo linalotolewa kwa ajili ya kuendeleza njia na fikra zake katika awamu mpya.