Nchini Sudan, jeshi lipo tayari kupokea mapendekezo ya kumaliza vita, kutoka kwa Marekani, iwapo wanamgambo wa RSF watajiondoa kwenye miji yote wanayodhibiti, wakati huu vita vikiendelea kwa mwaka wa tatu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nyaraka za siri, ambazo Shirika la Habari la Reuters limeona, na kuthibitishwa na viongozi waandamizi wa Sudan, zinaeleza kuwa,Marekani mwezi Juni ilipendekea mkataba kwa pande zote mbili, ili kusitisha vita kwa siku 90 kwa sababu za kibinadamu.

Wakati wa usitishwaji vita, mazungumzo yanatarajiwa kuendelea kwa lengo la kupata mkataba wa kudumu, kati ya jeshi na wanamgambo wa RSFna kuiwezesha Sudankupata uongozi wa kiraia kupitia uchaguzi.

Aidha, katika mapendekezo hayo, Umoja wa Mataifa, umetakiwa kuongoza mchakato wa wanamgambo wa RSF kujiondoa kwenye maeneo ya Kaskazini mwa Darfur, ambako waliuteka mji wa al-Fashir hivi karibuni.

Ripoti zinasema jeshi linaloongoza serikali ya Sudan kwa kiasi kikubwa limekubali mapendekezo haya, lakini inataka kuondolewa kwa wanamgambo wa RSFkatika maeneo wanayodhibuti.

Hii sio mara ya kwanza kwa Marekanikuja na mapendekezo ya kumaliza vita vinavyoendelea nchini Sudan kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *