
Madaktari, wauguzi, na wanaharakati wa haki za binadamu mepama leo walikusanyika nje ya Nje ya Chuo cha Kifalme cha Tiba na Mafunzo ya Afya ya Mtoto jijini London Uingereza wakipinga hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kumtia nguvuni kinyume cha sheria Hussam Abu Safiya daktari wa watoto Mpalestina.
Madaktari, wauguzi na wanaharakati wa haki za binadamu wamewasilisha ombi lao wakikihimiza chuo hicho cha afya kushinikiza hadharani ili kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Dakta Abu Safiya na wafanyakazi wengine wa afya wa Kipalestina wanaoshikiliza katika magereza ya Israel.
Waandaaji wa mkusanyiko huo wamesema kuwa Chuo hicho cha Kifalme cha Tiba na Mafunzo ya Afya ya Mtoto jijini London ambacho kinawakilisha maelfu ya wataalamu wa afya ya mtoto nchini Uingereza na duniani kote kinapasa kutumia ushawishi wake kuwatetea na kuwahami madaktari wenzao wa watoto wanaofanya kazi katika eneo iliyoathiriwa na mizozo ya kivita.
Wamesema, ukimya wa taasisi kuu za tiba unahatarisha kuhalalishwa mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa sekta ya afya na hospitali hasa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Naye mbunge wa chama Labour John McDonnell amesema kuwa na hapa ninamnukuu: “Naomba niiishi muda mrefu ili nimshuhudie Netanyahu mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Madaktari, wauguzi na wanaharakati wa haki za binadamu wameandamana mbele ya chuo hicho cha the Royal College of Pediatrics and Child Health jijini London huku mashirika ya kimataifa yakiendelea kubainisha wasiwasi kuhusu athari za vita vya mauaji ya kimbari kwa sekta ya afya ya Ukanda wa Gaza.