
Wataalamu wa mambo ya kale (wanaakiolojia) wamechimbua kaburi lenye umri wa miaka 3,000 karibu na jiji la Luxor kusini mwa Misri, mamlaka imetangaza siku ya Jumapili, Julai 12. Utambulisho wa mtu aliyefariki na kuzikwa katika kaburi hilo bado haujulikani, lakini jina lake limegunduliwa.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kaburi lenye umri wa miaka 3,000 ni ugunduzi wa kihistoria unaoonekana nchini Misri na maeneo mengine duniani. Katika nchi ya Misri, wataalamu wa mambo ya kale (wanaakiolojia) wamegundua makaburi kadhaa ya kipindi hiki, pamoja na makaburi ya viongozi wa jeshi na vitu vya thamani kama upanga wa kale.
Kaburi hilo, la mtu anayeitwa Paser, liligunduliwa na misheni ya Uholanzi kutoka Chuo Kikuu cha Leiden katika eneo la Theban pecropolis la jmbo la Gourna, kulingana na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri.
Wataalamu wanabainisha, kulingana na mtindo wa kipekee wa kisanii wa maandishi yake, kwamba kaburi hilo linatokana na kipindi cha Ramesside, ambacho kinaanzia Enzi za 19 na 20.
Likiwa magharibi mwa eneo linalojulikana la mazishi, linafuata mpangilio wa kitamaduni wa makaburi ya kibinafsi ya Theban kutoka Ufalme Mpya (1570-1069 KK): ua ulio wazi unaoelekea kwenye kanisa lililochongwa kwenye mwamba katika umbo la “T” iliyogeuzwa, lenye vyumba vya mazishi vilivyochongwa chini ya ardhi.
Kipindi cha miaka ya 1570–1069 KK (Kabla ya Kristo) kinajulikana kama Ufalme Mpya wa Misri (New Kingdom). Huu ulikuwa wakati wa dhahabu ambapo Misri ilikuwa himaya yenye nguvu zaidi duniani, iliyotawala maeneo makubwa kutoka Nubia (kusini) hadi Siria (kaskazini)
Wanakiolojia wamegundua mambo kadhaa ya usanifu yaliyohifadhiwa vizuri katika ua, ikiwa ni pamoja na kiti cha matofali ya matope kilichokusudiwa kubeba jiwe linakoandikwa majina, tarehe ya kuzalia na tarehe ya kufariki ya marehemu na ngazi zinzoshikiliwa na ngazi za pembeni zinazoelekea kwenye mlango.
Paser alikuwa nani?
Ndani, maandishi yenye jina la Paser yanamwonyesha akiabudu miungu mbalimbali katika madhabahu, na pia ameketi na mkewe mbele ya meza ya sadaka. Timu ya uchimbaji imebanisha kwamba inaendelea na juhudi zake za utafiti na kuweka kumbukumbu ili kubaini utambulisho wa Paser na kupata uelewa bora wa kipindi cha kihistoria na kiakiolojia.
Ugunduzi huu karibu na Luxor, mojawapo ya maeneo muhimu zaidi ya kiakiolojia duniani, unakuja huku Misri ikijaribu kutangaza uvumbuzi mpya ili kuongeza utalii, chanzo muhimu cha fedha za kigeni.