
Ndege mbili za zilitumwa kwa mara ya kwanza katika eneo la Paris kupambana na moto “mkali sana” siku ya Jumapili, Julai 12, katika msitu maarufu wa Fontainebleau, yapata kilomita hamsini kusini mwa mji mkuu wa Ufaransa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Moto huo ni wa “kiwango cha juu sana,” alisema Jumapili jioni naibu mkuu wa eneo hilo, Yannis Bouzar. Wazima moto wapatao 400 wanafanya kazi ya kupambana na moto huo, ambao, muda mfupi baada ya usiku wa manane, ulikuwa umeunguza takriban heka 800 na bado “unaendelea kuenea,” ameongeza wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Moto huo umesababisha kufungwa kwa sehemu ya barabara kuu ya A6, barbara kuu inayoelekea kusini mwa nchi, na usafiri kwenye reli ya mwendo kasi Kusini-mashariki “imevurugwa,” amesema Waziri wa Uchukuzi Philippe Tabarot.
Moto huo katika msitu wa Fontainebleau ulianza Jumapili alasiri kando ya A6, kabla ya kuenea msituni. Ni “mkali sana,” na ndege mbili za Dash bombardiers kutoka kusini mwa Ufaransa zimetumwa kutoka Bordeaux na NĂ®mes kusaidia kuudhibiti. Hata hivyo, helikopta na ndege zinazorusha maji zilizoletwa kutoka kusini kusambaza vidhibiti vya moto zililazimika kusitisha shughuli zao usiku.
Hii ni mara ya kwanza ndege kama hizo kutumika katika eneo la Paris, Luteni Kanali Eric Brocardi, msemaji wa Shirikisho la Kitaifa la Wazima Moto la Ufaransa, ameliiambia shirika la habari la AFP. Helikopta mbili, ndege moja, na wazima moto zaidi ya mia moja pia wako eneo la tukio, ameongeza. “Lengo ni kuokoa maisha na mali,” Brocardi amesema baadaye jioni.
Joto kali, ambalo limekuwa likizuia hewa katika eneo la Paris haswa kwa siku kadhaa, huongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuzuka kwa moto wa nyika.