Wajumbe watatu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamewasili jijini Goma wiki hii, kuthathmini utekelezwaji wa mkataba wa kusitisha vita kati ya waasi kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi hao wa serikali ya Kinshasa, waliwasili Goma kwa msaada wa ndege za MONUSCO kwa mujibu wa mikataba ya Doha na Washington.

Wawakilishi hao wa serikali ya DRC waliowasili Goma ni pamoja na Cosmas Ben Epule, Fredy Lokuli na André Kitoko ambaye ni Luteni Kanali katika jeshi la FARDC.

Naibu mwakilishi wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC Vivian van de Perre, amesema wajumbe hao wamekuja Goma , kuiwakilisha serikali katika kuthathmini mwenendo wa utekelewaji wa maelewano ya usitishwaji vita.

Waasi wa AFC/M23, Tarehe 19 Mei 2026.
Waasi wa AFC/M23, Tarehe 19 Mei 2026. AFP – JOSPIN MWISHA

Kazi ya wajumbe hao ni kuthatmini na kuripoti namna utekelewaji huo unavyoendelea kati ya serikali ya Kinshasa na waasi AFC/M23, huku ajenda kubwa ikiwa ni namna ya kuwalinda, raia wa kawaida, kuweka silaha chini miongoni mwa masuala mengine.

Licha ya kuwepo kwa mkataba wa amani wa Washington, ambao ulitiwa saini mwaka mmoja uliopita, mapigano yameripotiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa AFC/M23 ikiwemo wilaya ya Masisi wiki hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *