
Shirika la afya duniani WHO, limesema idadi kamili ya walioambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huenda ikawa mara nne zaidi kuliko takwimu rasmi zinavyoonesha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, zaidi ya watu 1,960 wameambukizwa huku wengine zaidi ya 700 wakifariki tangu ugonjwa huo ulipotangazwa miezi miwili iliyopita.
Hata hivyo, mkurugenzi wa dharura wa WHO Chikwe Ihekweazu, amewaambia waandishi wa habari kuwa, tathmini ya hesabu inaonesha ukubwa wa mlipuko huu wa 17, ni angalau mara mbili hadi nne ya idadi ya matukio kamili, baada ya kuripotiwa katika majimbo matano, asilimia 90 ikiwa katika eneo la Ituri.
Virusi aina ya Bundibugyo havijapata dawa wala chanjo, Ihekweazu akisema jambo la kutisha zaidi ni kwamba matukio mengi yaliyoripotiwa hivi karibuni, yanahusu watu waliofariki kabla ya kufika kwenye kituo cha afya au kupata matibabu.
Hata hivyo mkurugenzi huyu amesema ametiwa moyo na kuongezeka kwa uwezo wa matibabu kila wiki licha ya kwamba katika siku chache zilizopita, kulikuwa na matukio zaidi ya 80 yaliyothibitishwa kila siku.