
Ndoto ya timu ya taifa ya soka ya Ufaransa kushinda kombe la dunia, imegonga mwamba, baada ya kufungwa na Hispania, mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa siku ya Jumannne usiku jijini Arlington nchini Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ilikuwa mechi ngumu kwa wachezaji wa Ufaransa, na huzuni kubwa kwa mashabiki baada ya Mikel Oyarzabal kufungua safu ya mabao katika dakika ya 22 kupitia mkwaju wa penalti huku Pedro Porro akifunga bao la pili katika dakika ya 58, huku jitihada za Ufaransa, kutafuta bao zikiambulia patupu.
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps, ambaye anatarajiwa kuondoka katika nafasi yake, amesema baada ya kupoteza mchuano huo, wachezaji wake waliachwa na Mawazo, huku wakimlaumu mwamuzi wa kati Ivan Barton kutoka El Salvador.
Ufaransa imeondoka kwenye michuano hiyo baada ya kufunga mabao 16 katika mechi sita ilizocheza, baada ya ndoto ya kushinda kombe la dunia kwa mara ya tatu kuyeyuka.
Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yaliyokuwa yamepewa nafasi kubwa ya kufika fainaili na kushinda kombe la dunia, kwa sababu ya vipaji vya wachezaji wake, lakini ililemewa na Hispania.
Le Bleus, sasa itacheza siku ya Jumamosi, kumtafuta mshindi wa tatu, kati ya Uingereza au Argentina, baada ya mechi ya nusu fainali ya Jumatano.