Askari wapya wa Depo Na. K3 mkoani Rukwa wameamua kutenga sehemu ya mshahara wao wa kwanza baada ya kuajiriwa ili kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule ya Msingi Malangali, Manispaa ya Sumbawanga.

Kupitia mchango huo, askari hao walikabidhi vifaa na vyakula kwa wanafunzi hao katika hafla iliyoongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kamanda Masija amesema hatua hiyo inaakisi dhamira ya Jeshi la Polisi ya kuimarisha uhusiano na jamii kupitia shughuli zinazogusa makundi yenye mahitaji maalum.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *