Dar es Salaam. Kauli ya Haji Manara ya kumzawadia mama mzazi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Mama Dangote, kiasi cha Sh40 milioni katika sherehe ya kuzaliwa kwake, bado imeendelea kuzua mjadala mkubwa, huku wengi wakijiuliza kama fedha hizo zilikabidhiwa kweli au zilibaki kuwa ahadi mbele ya wageni.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia Julai 12, 2026, Manara alichukua kipaza sauti na kumuita mwanamuziki Ommy Dimpoz, akimtaka aende kwenye gari lake kuchukua kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumkabidhi Mama Dangote.

“Nenda kwenye gari yangu ukachukue milioni 40 kwa ajili ya Mama,” amesema Manara mbele ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Hata hivyo, Ommy Dimpoz alionekana kucheka badala ya kwenda kuchukua fedha hizo, jambo lililowafanya baadhi ya watu kushindwa kufahamu kama Manara alikuwa akizungumza kwa utani au alimaanisha kile alichokisema.

Baada ya tukio hilo, Mwananchi lilimuuliza Diamond Platnumz iwapo Mama yake tayari alikuwa amepokea fedha hizo.

Badala ya kujibu moja kwa moja, Diam ond alitabasamu na kucheka, bila kuthibitisha wala kukanusha kama kiasi hicho cha fedha kilifika mikononi mwa Mama Dangote.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Haji Manara, Mama Dangote au Diamond Platnumz zinazothibitisha kuwa fedha hizo zilikabidhiwa.

Ukimya huo umeendelea kuwapa nafasi watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoa maoni tofauti kuhusu tukio hilo. Wapo wanaoamini Manara alikuwa akitania ili kuongeza burudani kwenye sherehe hiyo, huku wengine wakisisitiza kuwa kutokana na ukarimu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *