#HABARI: Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza Shilingi bilioni 2.8 katika miradi mitatu mikuu ya maendeleo wilayani Gairo.

Fedha hizo zimetumika kujenga Kituo cha Afya Chanjale (Shilingi milioni 680), kuboresha Barabara ya Confort Pub–Magoweko (Shilingi milioni 470), na kujenga Shule ya Amali Kwipipa (Shilingi bilioni 1.6) ili kusogeza huduma bora karibu na wananchi.

Uwekezaji huo umebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa ziara yake ya kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi hiyo.
Prof. Shemdoe amesema kuwa kiasi hicho ni sehemu ya zaidi ya Shilingi bilioni 100 zilizotolewa na serikali katika Halmashauri ya Gairo tangu Rais Samia aingie madarakani.

Viongozi wa eneo hilo, akiwemo Mbunge wa Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby, na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Josephine Kapoma, wamepongeza juhudi hizo wakieleza kuwa Shule ya Amali Kwipipa, inayofundisha masuala ya uhandisi, itakuwa chachu ya kupata wataalamu wazawa wenye ujuzi na kuboresha mazingira ya elimu ya ufundi nchini.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *