Zaidi ya watu milioni 3.7 nchini Madagascar wanatarajiwa kukabiliwa na njaa kali huku hatari ya utapiamlo ikiongezeka miongoni mwa watoto na makundi yaliyo katika mazingira magumu.

Shirika la Save the Children limeripoti kuwa njaa nchini Madagascar inatarajiwa kuwa mbaya zaidi baadaye mwaka huu, huku idadi ya watu wanaosumbuliwa na viwango vya hatari vya uhaba wa chakula ikitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 75.

Takriban watoto 502,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano au mtoto mmoja kati ya kila watoto 10 nchini Madascar pamoja na wanawake 21,000 wajawazito na wanaonyonyesha upo uwezekano wakakabiliwa na utapiamlo mkali kati ya Mei 2026 na Aprili mwaka ujao.

“Hii inajumuisha takriban watoto 78,000 wanaotarajiwa kuwa na utapiamlo mbaya zaidi unaohitaji matibabu ya dharura,” imeeleza taasisi ya Kimataifa Inayoshughulikia njaa duniani.

 Ripoti hiyo pia imekadiria kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na viwango vya njaa vilivyo katika hali ya hatari kubwa kati ya mwezi Oktoba mwaka huu hadi Februari mwakani inaweza kukuongezeka hadi kufikia milioni 3.72, au takriban asilimia 10 ya idadi ya watu, huku karibu watu 426,000 wakitarajiwa kukabiliwa na hali ya dharura; idadi ambayo ni zaidi ya mara mbili ya ile ya sasa.

Shirika la Save the Children limeitaka jamii ya kimataifa kuongeza  ufadhili wa dharura wa kibinadamu ili kukidhi misaada ya chakula, huduma za lishe, huduma za afya na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa familia zilizo katika mazingira magumu kuwa mbaya zaidi,” ameeleza Tatiana Dasy, mwakilishi wa shirika hilo nchini Madagascar, akitoa maoni yake kuhusu ripoti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *