MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali, amesema dirisha la usajili wa wachezaji kuelekea msimu wa 2026-2027 linafunguliwa Julai 20, 2026 na kufungwa Septemba 5, 2026, hivyo litadumu kwa takribani siku 47.

Issa amesema usajili huo utahusisha washiriki wote wa mashindano yanayosimamiwa na bodi hiyo kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya hadi Taifa huku akizitaka klabu zikamilishe usajili ndani ya muda uliopangwa.

“Hatutakuwa na muda wa nyongeza baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, hivyo nasisitiza timu kutumia muda huo vizuri uliotengwa kuepuka changamoto wakati wa mashindano,” amesema. 

Ameeleza kuwa, kipindi hicho kitatoa fursa kwa timu kusajili wachezaji wapya, kufanya uhamisho pamoja nyaraka muhimu zinazohitajika kwa mujibu wa kanuni za mashi ndano. Vilevile, amesema Bodi ya Ligi imekamilisha maandalizi ya awali ya msimu mpya na kwasasa inaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kuzing atia kanuni, sheria na ratiba zilizopangwa.

Usajili huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa 2026-2027 Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *