#MICHEZO: Naibu Waziri wa Michezo wa Zanzibar, Mheshimiwa Ali Abdulghulam Hussein, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kuhakikisha maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) yanakuwa bora na ya mfano.

Mhe. Abdulghulam ameeleza kuwa uzoefu walioupata kutoka kwenye mashindano makubwa ya kimataifa kama Kombe la Dunia umewasaidia kubaini maeneo ya kuboresha ili kuifanya michuano hiyo inayoratibiwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda kuwa ya mafanikio makubwa.

Mhe. Abdulghulam amefafanua kuwa mafunzo hayo yamejikita katika usimamizi wa wageni, uimarishaji wa usalama, usafi, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kujipatia fursa za kiuchumi.

Amebainisha kuwa Serikali inatumia masomo yote hayo kwa vitendo katika maandalizi ya AFCON 2027 ili kuwezesha nchi kunufaika kikamilifu na uenyeji wa michuano hiyo.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *