
Umoja wa mataifa umeonya kuhusu hatari ya virusi vya Ebola kuenea katika kambi zinazotoa hifadhi kwa watu waliokimbia vita mashariki mwa DRC, kutokana na hali ya msongamano inayochochea msambao wa ugonjwa huo ambao umekithiri katika majimbo matano nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la kuratibu misaada la umoja huo, OCHA limesema maambukizi ya ebola yamethibitishwa katika kambi 16 katika jimbo la Ituri ambalo ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Kulingana na UN, kambi hizo zinatoa hifadhi kwa zaidi ya watu laki mbili na elfu 70, ambao wanakabiliwa na changamoto ya msongamano na upatikanaji wa huduma za msingi hali inayohatarisha kuenea kwa ugonjwa huo.
Aidha OCHA inasema Pamoja na washirika wao, wamekuwa wakitengeneza vituo vya kunawa mikono Pamoja na kuwahamasisha wanajamii kuhusu hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Hata hivyo Ocha Inasema mahitaji ya kudhibiti ugonjwa huo yamezidi rasilimali iliopo na sasa shirika hilo linatoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia kufanikisha mwitikio wa ugonjwa huo pamojana msaada wa kuokoa maisha ya jamii zilizokimbia makazi yao kutokan ana vita.