Kampuni ya SUHARA Logistics Company Limited imesema ushiriki wake katika Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026) umeiwezesha kukutana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, kupanua mtandao wa kibiashara na kuongeza fursa za ukuaji wa kampuni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Mwanza , Meneja wa Miradi kutoka SUHARA Logistics Company Limited, Amina Abdallah, amesema kampuni hiyo inatoa huduma za usafirishaji wa mizigo kutoka eneo la chanzo hadi sehemu anayoelekeza mteja kwa kuzingatia viwango vya usalama na ubora.

Kwa upande wake, Mwangalizi wa Tawi la SUHARA Mkoa wa Mwanza, Sarah Utiku, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuandaa Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF 2026) na kuongeza kuwa Kampuni hiyo imechangia Maendeleo ya jamii ikiwemo kutoka Ajira kwa Wazawa.

Naye Mkurugenzi wa SUHARA Logistics Company Limited, Anand Barchha, amesema huduma za uhifadhi wa mizigo (warehousing) ni sehemu muhimu ya mnyororo wa ugavi katika ununuzi na usambazaji wa bidhaa, na kampuni imeweka mifumo na viwango bora vya usimamizi wa maghala na bidhaa .

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *