
Wakati huu wanasiasa wa upinzani na viongozi wa dini, wanaposubiri tangazo rasmi la rais, ili kuanza mazungumzo ya kitaifa, imebainika kuwa rais wa zamani wa Guinea, aluhusika pakubwa, kwenye mazungumzo yaliyopelekea rais Felix Tshisekedi kukubali mazungumzo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Alpha Condé hakuonekana kwenye picha zilizopigwa kwenye Ikulu ya rais jijini Kinshasa, wakati viongozi wa dini wakiongozwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO, walipotangaza utayari wa rais Tshisekedi kuhusu mazungumzo hayo, ripoti zinasema kiongozi huyo wa zamani wa Guinea, hakutana kuonekana hadharani.
Ripoti zaidi zinasema ushiriki wa Conde kwenye jitihada hizi, ulianza mapema mwezi Julai, na wakati mmoja alikutana na rais Tshisekedi jijini Brazzaville kwa ajili ya mazungumzo.
Aidha, alikutana pia na Kadinali Fridolin Ambongo, kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini DRC. Alpha Conde anaelezwa kuwa mshirika wa karibu wa rais Tshisekedi, na ushiriki wake ulitokana pia na ushauri uliotolewa na rais wa nchi Jirani ya Congo Brazaville Denis Sassou-Nguesso.
Hata hivyo, mpaka sasa haijawa wazi nafasi ya Alpha Conde, kwenye mazungumzo haya yanayotarajia kujadili masuala ya kisiasa, hasa mpango wa kubadilisha Katiba na hali ya utovu wa usalama Mashariki mwa DRC.