Nchi ya Marekani na Saudi Arabia zimetangaza makubaliano ya ushirikiano ya kihistoria yatakayopelekea kuundwa kwa mpango wa nyuklia wa kiraia katika taifa hilo la Ghuba.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makubaliaono hayo yaliopewa jina ya 123, yanalenga kusaidia taifa hilo la kifalme kuendeleza mpango wake wa nishati ya nyuklia, pia yanajumuisha makubaliano kuhusu hatua za ulinzi na usimamizi.

Ni makubaliano yanayofanyika wakati huu Marekani ikiendelea kuzozana na Iran, mzozo ambao kwa kiasi kikubwa ulianza kutokana na wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran, suala ambalo limesalia kikwazo hata kwenye mazungumzo yao ya amani.

Mpango wa nyukilia wa Iran umekuwa kizingiti kwenye mazungumzo yake na Marekani.
Mpango wa nyukilia wa Iran umekuwa kizingiti kwenye mazungumzo yake na Marekani. AFP – HAMED MALEKPOUR

Katika makubaliano hayo, Marekani inatarajia kunufaika kiuchumi kupitia uuzaji wa teknolojia ya nyuklia kwa Saudia na kuunda nafasi za ajira kwa Wamarekani.

Mkataba huo utawasilishwa katika bunge la Congress kwa ajili ya mapitio, hata hivyo hakuna uwezekano wa utekelezwaji wake kuzuiwa katika bunge hilo linalodhibitiwa na Republican.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *