Nchi wanachama 125 wa mahakama ya kimataifa ya ICC wanatarajiwa kukutana Ijumaa kuamua kuhusu hatma ya mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Karim Khan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Karim Khan alisimamishwa kazi kwa madai ya dhuluma ya kingono dhidi ya mmoja wa wafanyikazi katika Ofisi yake, madai ambayo anakanusha vikali.

Mwezi Mei mwaka wa 2025, Khan alijiondoa kwenye majukumu yake kama njia moja ya kushugulikia madai yaliotolewa dhidi yake na mfanyikazi huyo wa kike katika Ofisi yake baada ya uchunguzi kuanzisha dhidi yake mwaka wa 2024.

Uamuzi dhidi yake unatarajiwa kutolewa na wawakilishi wa nchi 125 wanachama wa ICC katika kura ambayo itapigwa kwa siri kwenye kikao cha faragha.

Nchi wanachama wa ICC zinatarajiwa kupiga kura kuamua hatma ya Khan.
Nchi wanachama wa ICC zinatarajiwa kupiga kura kuamua hatma ya Khan. REUTERS – Piroschka Van De Wouw

Khan anatuhumiwa kwa kumdhulumu Wakili raia wa Malaysia ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye Ofisi yake kama msaidizi wake wakati huo.

Khan, ambaye mwendesha mashtaka Mkuu wa ICC tangu mwaka wa 2021, amekanusha madai hayo.

Katika taarifa iliochapishwa kwenye mtandao wa X na mawakili wa Khan, wamewataka wanachama wa ICC kutomuondoa mteja wao kwenye wadhifa wake.

Mawakili wake wanasema hakupewa nafasi ya kujitetea kama inavyotakiwa katika kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *