
Kulingana na takwimu za mashirika ya kiraia, angalau raia 18 wameuawa siku ya Jumatano, Julai 22, 2026, katika shambulio jipya lililohusishwa na waasi wa Uganda wa ADF katika eneo la Mambasa la mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Shambulio hilo lililenga vijiji kadhaa katika eneo la Mambembe-Bella.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idadi hii ya vifo bado ni ya muda. Watu kadhaa bado hawajulikani walipo, na washambuliaji bado wanaripotiwa katika eneo hilo. Waathiriwa wengi wao ni wachimbaji dhahabu wanaofanya kazi katika eneo hili la uchimbaji madini. Baadhi wamechukuliwa mateka na kundi hili la wanajihadi.
“Idadi ya vifo huenda ikaongezeka,” anaonya Kambale Penzi Philemon, kiongozi wa mashirika ya kiraia. Anaiomba mamlaka kuwalinda watu na anaamini kwamba “adui anaendelea kuzurura kwa uhuru katika vijiji bila hofu yoyote.”
Kulingana na mwanaharakati huyu, waathiriwa kadhaa walikatwa vichwa kwa mapanga. Anaiomba serikali ya Kongo kuimarisha uwepo wa kijeshi na anarudia kwamba “kazi ya serikali ni kulinda watu na mali zao.” Pia anasikitishwa na ukosefu wa kuingilia kati kutoka kwa vikosi vilivyopo katika eneo hilo wakati wa shambulio hili. Hali hii ni inatia huzuni kwa sababu “kila siku, tunawazika watu wetu wanaouawa,” anasema.
“Hatujaona hata uingiliaji kati wa MONUSCO […] Inauma tunapowazika watu wetu wanaokufa kila siku”
Shambulio hili jipya ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi mabaya yaliyofanywa katika wiki za hivi karibuni na ADF, kundi lenye silaha ambalo limeahidi utii kwa Dola la Kiislamu, katika eneo la mpaka kati ya mmikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini.