Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC), kikosi chenye nguvu cha Jamhuri ya Kiislamu, leo Ijumaa kimewataka raia katika Mashariki ya Kati kukaa mita 500 mbali na eneo lolote linalohifadhi vikosi vya Marekani, katikati ya ongezeko la mashambulizi na Washington.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tunawasihi wakazi wa nchi ambazo wanajeshi wa Marekani wamenapiga kamb, kukaa mita 500 mara moja kutoka kwenye maficho yao, ili wawe salama,” IRGC imesema katika taarifa iliyorushwa kwenye televisheni ya serikali, huku Iran ikishambulia mataifa jirani ya Ghuba kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Marekani.

Marekani imezindua mfululizo mpya wa mashambulizi ya anga nchini Iran siku ya Ijumaa, Julai 24, shambulio lake la kumi na tatu mfululizo. Waziri wa mambo ya nje wa Iran ametangaza kwamba nchi yoyote inayoisaidia Marekani katika mashambulizi yake “itabeba jukumu la kimataifa la pande zinazohusika.”

Wakati huo huo waasi wa Houthi, washirika wa Iran, wamefungua vita vya pili katika mzozo huo, wakidai kuhusika na mashambulizi katika Bahari Nyekundu ambayo yamesababisha bei ya mafuta kuwa juu ya dola 100 kwa pipa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *