Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikisha upandikizaji wa vifaranga vya samaki sato milioni 1.5 katika Ziwa Rwakajunju wilayani Karagwe.����
Akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Wilaya ya Karagwe, Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa amesema wanaiomba Serikali iwasaidie kupata nyongeza ya vifaranga vya samaki kufikia milioni 5 sambamba na kupatiwa boti ya doria kwa lego la kuongeza ulinzi na usalama wa Mradi huo.
����Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Nazael Madalla ameeleza kuwa Serikali itaongeza vifaranga katika Ziwa Rwakajunju pamoja na kufanya upimaji wa ziwa hilo ili kubaini kama linafaa kwa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.��
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ameishukuru Serikali kwa kuleta vifaranga milioni 1.5 vyenye thamani ya shilingi milioni 450.����
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)