Jumla ya wapanda mlima 55 kwa njia ya miguu na baiskeli wameanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia kampeni ya GGM Kili Challenge yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.
Wapanda mlima hao ambapo 42 ni wapanda kwa miguu na 13 kwa njia ya baiskeli wameagwa na kukabidhiwa bendera za taifa na Mkuu wa Wilaya ya Hai ( DC) mheshimiwa Hassan Bomboko kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ( RC) Mheshimiwa Nurdin Babu.
Naye Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayehusika na Miradi endelevu na Mahusiano barani Afrika Bw. Simon Shayo amesema kuwa mgodi wa Geita unajisikia fahari kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mashirika, taasisi na Serikali katika kufanikisha jambo hili kwa zaidi ya miongo miwili.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho amesema kampeni hiyo kwa kiasi kikubwa imesaidia vita dhidi ya Ukimwi na kuwataka wadau wengine wajitokeze na kuiunga mkono.
Tukio la upandaji mlima limeenda sambamba na zoezi la upandaji miche ya miti 5000 iliyotolewa na GGML kuzunguka maeneo ya mlima kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.
(Feed generated with FetchRSS)