Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Kaster Ngonyani, amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kufichua vitendo vya uhalifu, akisisitiza kuwa usalama wa jamii unategemea ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi.

Ngonyani ametoa wito huo wakati akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa katika Kituo cha Afya Ilembo, akieleza kuwa wananchi hawapaswi kuliona Jeshi la Polisi kama chanzo cha hofu, bali mshirika muhimu katika kudumisha amani na usalama.

Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *