Nchini Mali, wakazi 5,000 wa Kouakourou, katika wilaya ya Djenné katikati mwa Mali, wote wametoroka kijiji chao. Kufuatia shambulio la wanajihadi wa JNIM, kundi linalohusishwa na Al Qaeda, mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo jeshi la Mali lilishindwa, wanajihadi hao waliwaamuru wakazi hao kuondoka mji huo. Sasa ni wakimbizi wa ndani, wanapewa hifadhi na familia zao na wengine wanapewa hifadhi na serikali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na timu ya wahariri ya RFI ya Mandinka na Fulfulde,

Nchini Mali, Jumamosi, Julai 18, 2026, JNIM ilishambulia na kuchukuwa udhibiti wa kambi ya kijeshi ya Kouakourou. Siku iliyofuata, wanajihadi walidungua helikopta ya jeshi. Wanajeshi kadhaa waliokuwa wamevaa nguo za kiraia walikamatwa walipokuwa wakijaribu kujichanganya na raia. Kuhusu wanakijiji, wanajihadi waliwaamuru waondoke kijijini mwao.

Taarifa hii imethibitishwa na viongozi wengi wa eneo hilo na wakazi wa Kouakourou.

Msafara walazimika kurudi nyuma Djenné

Tangu mwanzoni mwa wiki, jeshi limefanya mashambulizi ya anga katika eneo hilo, likidai siku ya Jumanne, Julai 21, “kuwaua magaidi watano” waliokuwa kwenye pikipiki na kuharibu “gari lililojaa vifaa vya kijeshi.”

Wanajeshi wengine pia walitumwa, lakini msafara, unaojumuisha wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Urusi kutoka Kikosi cha Africa Corps, haukufika Kouakourou, ulilazimika kurudi nyuma. Mashambulizi ya kuvizia, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, uharibifu wa daraja: wapiganaji wa jihadi walilazimisha jeshi kurudi nyuma hadi Djenné.

Wanapewa hifadhi katika shule

Kuhusu wakazi wa Kouakourou, wote wamekimbilia katika vijiji vya jirani vya Pora au Saba, ambapo hupewa msaada wa kimaadili licha ya hali ngumu inayowakabili wakazi wa mji huo, au hadi Djenné, karibu kilomita 40, ambapo baadhi ya wakazi walilazimika kusafiri kwa miguu.

Katika mji wa Djenné, wanafikia mamia kadhaa – wanaume, wanawake, na watoto – wakiishi na familia au wakihudumiwa na mamlaka katika shule ya mji huo. Tani vyakula na vyandarua vimewasilishwa na Kurugenzi ya Kitaifa ya Maendeleo ya Jamii. Michango inaendelea kupokelewa. Baadhi ya wakazi wamesafiri hadi mji mkuu, Bamako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *