Vinicius Jr

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 1

Arsenal inafikiria uwezekano wa kumsajili winga wa Brazil, Vinicius Jr, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 asipoongeza mkataba wake na Real Madrid. (Athletic -usajili unahitajika)

Kocha mpya wa Real Madrid, Jose Mourinho, huenda akapinga jaribio lolote la Arsenal kumsajili Vinicius msimu huu wa joto, kwani kocha huyo raia wa Ureno ameuambia uongozi wa klabu kuwa anataka kusalia na wachezaji wake wote wakuu (Telegraph – usajili unahitajika)

Arsenal iko tayari kuvunja rekodi ya uhamisho nchini Uingereza ili kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Atletico Madrid. (Teamtalk)

Inter Milan ina nia ya kumsajili beki wa Argentina, Cristian Romero, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Tottenham. (Sky Sports)

RB Leipzig imekataa ofa ya pauni milioni 85.4 ya klabuya Real Madrid kwa ajili ya kumsajilia winga wa Ivory Coast, Yan Diomande. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 pia ananyatiwa na klabu za Liverpool na Manchester City, miongoni mwa nyinginezo. (Sky Sports)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *