China imetangaza Jumamosi, Januari 24, ufunguzi wa uchunguzi dhidi ya mmoja wa maafisa wakuu katika jeshi lake kwa “ukiukaji mkubwa wa nidhamu,” neno la kawaida la ufisadi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Baada ya ukaguzi, imeamuliwa kufungua uchunguzi dhidi ya Zhang Youxia,” mmoja wa makamu wenyeviti wa Tume Kuu ya Jeshi (CMC), tume yenye nguvu nchini China, na pia dhidi ya Liu Zhenli, afisa mwingine wa cheo cha juu, Wizara ya Ulinzi imetangaza katika taarifa.

MCC ambayo inaongozwa na Rais Xi Jinping inasimamia udhibiti kamili wa chama juu ya jeshi na kuratibu ulinzi wa taifa. Tume hiyo ina makamu wawili wenyeviti. Kutokana na uzoefu na hadhi yake, Zhang Youxia kwa ujumla anachukuliwa kuwa mwenye nguvu zaidi. Makamu wa pili wa mwenyekiti, Zhang Shengmin, alirithi nafasi hiyo mwezi Oktoba baada ya kuondolewa kwa He Weidong, baada yakutangazwa uchunguzi kuhusu ufisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *