Dar es Slla. Clatus Chotta Chama, amerudi tena Msimbazi. Pale ndo ‘homu’ kwake kwa hapa Bongo. Simba ni chama lake la rohoni na katika hili hana ujanja kuikataa ikimtaka. Ni ukweli uliowazi kuna huba zito la Chama na Simba.

Na Simba huyu Chama ndo ‘staa’ wao mkubwa kuwahi kutokea. Na hawana ujanja wanapolisoma jina lake. ‘Mwamba wa Lusaka’ Clatous Chotta Chama, mioyo inawaruka kinoma. Wana ndoa ya rohoni.

Simba wanampenda Chama na Chama anawapenda Simba. Hata uzi mwekundu hukaa mwilini kwa Chama vizuri kuliko uzi mwingine. Simba wapo kwenye ‘hadi taim’ na wanahitaji huduma ya Chama. 

Chama yupo kwenye ‘hadi taim’ pia, anahitaji kuwepo Unyamani. Ni kama mwanadada Kajala vile mbele ya Konde Boy. Kwa pamoja wanahitajiana kwa penzi ili mishe ziende, uhusiano wao unawapa pesa zaidi.

Konde akiona ‘viprojekti’ vyake vinasuasua lazima ajisogezea kwa Kajala. Ukweli ni kwamba siku zote Konde Boy nyota yake hung’ara zaidi akiwa na Kajala. Kama enzi za Diamondi na Wema nyakati zile.

Kajala pia mishe zake za kuunga unga kwa sasa, anahitaji kuwa ‘araundi’ na Konde Boy. Maana hata yeye akiwa na dogo hilo la Kimakonde, nuru yake huwaka sana. Wanahitajiana kwa kifupi na halina ubishi.

Kinachoendelea Unyamani pale, Simba na Mwamba wa Lusaka ni A. Na kinachoendelea  kwa Konde na Kajala ni B. Kuna mfanano kati ya penzi la Kajala na Konde Boy ni kama penzi la Simba na Chama. Ndio ukweli huo. 

Hivi sasa Konde Boy karudiana na Kajala wake kama mara ya tatu. Simba wamerudiana na Chama wake kama mara ya tatu sasa. Ni wazi penzi la Simba na Chama ni kama Konde Boy na Simba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *