UNMISS imeonya kuwa vitisho hivyo vinaweka jamii ambazo tayari ziko hatarini katika hatari kubwa zaidi na vinaweza kudhoofisha zaidi uthabiti wa nchi.

UNMISS imesema jamii katika jimbo la Jonglei na maeneo mengine ya Sudan Kusini zinaendelea kuteseka kwa madhara makubwa kutokana na kuongezeka kwa mgogoro, ikiwa ni pamoja na mapigano ya moja kwa moja kati ya vikosi vinavyohusishwa na pande kuu za makubaliano ya amani.

Ujumbe huo umesisitiza kuwa raia wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa mapigano hayo, licha ya ahadi zinazorudiwa mara kwa mara na viongozi kwamba mchakato wa amani unaendelea.

Kusitisha uchochezi na kutimiza ahadi za amani

“Kaui za uchochezi zinazohimiza vurugu dhidi ya raia, wakiwemo walio hatarini zaidi, ni za kuchukiza kabisa na lazima zikome mara moja,” amesema Graham Maitland, Afisa Anayesimamia UNMISS, akisisitiza kuwa uchochezi wa vurugu unadhoofisha juhudi za ulinzi wa raia na kuchochea zaidi watu kufurushwa na mateso.

Wakati viongozi wa Sudan Kusini wanaendelea kusisitiza kujitolea kwao kwa amani, UNMISS imebainisha kuwa mapigano na ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano vinaendelea bila kukoma katika maeneo mbalimbali ya nchi. Ujumbe huo umeonya kuwa pengo kati ya kauli za kisiasa na hali halisi uwanjani linahatarisha imani ya wananchi na linaweza kurudisha nyuma mafanikio madogo yaliyopatikana tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya amani.

“UNMISS inawahimiza viongozi wa nchi kuweka maslahi ya wananchi wao mbele kwa kusitisha mapigano na kuheshimu ahadi walizozitoa chini ya makubaliano ya amani,” amesema Maitland.

Ameongeza kuwa hilo linapaswa kujumuisha “kurejea katika maamuzi kwa pamoja, kuheshimu mipango ya kugawana madaraka, na kukubaliana juu ya njia ya wazi na shirikishi ya kumaliza kipindi cha mpito kwa amani”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *