Mashambulizi hayo dhidi ya baadhi ya vituo muhimu vya makazi ya watu nchini Ukraine, ambayo yanaripotiwa kuhusisha takribani droni 400, pia yamewaacha maelfu ya watu bila umeme, mitambo ya upashaji joto na maji.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA limesema halijoto nchini humo imeshuka hadi nyuzi joto -20 Celsiasi, na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati yameacha familia katika hali ya kuganda kwa baridi.

Wazee na wenye ulemavu wanakwama majumbani

Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa Watu wengi wazee na watu wenye ulemavu mara nyingi hukwama majumbani mwao katika majengo marefu ya ghorofa bila umeme na joto, hawawezi kupika chakula cha moto au kuchaji vifaa vyao ili kuendelea kuwasiliana.

Mashambulizi ya hivi karibuni yamefanyika wakati mazungumzo ya amani yakiendelea katika Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu (UAE), yakihusisha wajumbe kutoka Urusi, Ukraine na Marekani.

Katika mji wa Ukraine wa Kharkiv, bweni lililokuwa linawahifadhi watu waliokimbia mapigano kwenye mstari wa mbele lilishambuliwa. Hospitali na majengo ya makazi pia yameharibiwa.

Katika mji mkuu Kyiv, maelfu ya majengo ya ghorofa ambayo yalikuwa yanaanza kurejeshewa huduma za msingi baada ya wimbi la awali la mashambulizi ya Januari 9 na 20, yamekatikiwa tena umeme wakati wa baridi kali.

Majengo ya majengo yaliyoharibiwa huko Saltivka, Kharkiv, Ukraine, yenye ardhi iliyofunikwa na theluji na uwanja wa michezo katika eneo la mbele.

© UNHCR/Yevheniia Kozun

Mabomu ya majengo ya makazi huko Saltivka, Kharkiv, yamewaacha Waukrainia wengi bila umeme.

Maelfu ya watu wako gizani

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema Jiji zima la Chernihiv na mamia ya maelfu ya familia katika eneo linalolizunguka wamebaki bila umeme.

Timu za ukarabati na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanaendelea kufanya kazi katika halijoto ya chini kusaidia waathirika.

Kwa mujibu wa duru za vyombo vya habari, zaidi ya watu milioni moja hawana umeme kote nchini, takribani 800,000 kati yao wakiwa Kyiv.

Bwana. Schmale, katika taarifa amesisitiza kuwa “Mzunguko huu wa kimfumo wa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati unakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na lazima ukome.”

Ameongeza kuwa Raia wa Ukraine wanapaswa kuishi majumbani mwao kwa usalama na joto, si kwa hofu ya duru nyingine ya uharibifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *