Pamoja na Yanga kupoteza mchezo uliopita ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa mabao 2-0, hesabu za kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo bado ziko hai kwa upande wao.

Pointi nne ambazo imeshakusanya hadi sasa kwenye Kundi B la mashindano hayo, zinaifanya Yanga iendelee kubakia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lake linaloongozwa na Al Ahly yenye pointi saba huku FAR Rabat iliyo nafasi ya tatu na JS Kabylie inayoshika mkia kila moja ikiwa na pointi mbili.

Hata hivyo kama ndoto za Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu zitatimia, Kipa Djigui Diarra atakuwa miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia timu mbili za Kaskazini mwa Afrika kutoingia robo fainali.

Ikumbukwe kundi hilo lina timu nne na tatu ni za Kiarabu ambao kama Yanga ikinyakua nafasi moja ya kwenda robo fainali, pasipo shaka yoyote, timu mbili za Uarabuni lazima ziage mashindano hayo.

Takwimu za mechi mbili ambazo zimeipa Yanga pointi nne kabla ya kutoka sare na Al Ahly, zinaonyesha pasipo uhodari wa Diarra, leo hii Yanga ingekuwa kama Watani wao Simba ambao hadi sasa hawana pointi yoyote katika mechi tatu walizocheza hadi sasa za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ukiondoa mchezo dhidi ya Al Ahly juzi, katika mechi mbili za mwanzo ambazo ni dhidi ya AS FAR na JS Kablie, Diarra ameokoa idadi ya michomo nane ambayo kama robo yake tu ingeingia wavuni, leo Yanga ingekuwa mkiani mwa kundi hilo.

Mechi ya kwanza dhidi ya FAR Rabat katika Uwanja wa nyumbani wa New Amaan Cross, Diara aliokoa nafasi moja ya wazi ambayo kama Waarabu hao wangefunga, maana yake hiii leo, Yanga ingekuwa inategemea maajabu ili ifuzu robo fainali.

Katika mchezo wa Yanga dhidi ya JS Kabylie, Diarra alizuia mashambulizi sita ya wapinzani yasiingine wavuni. Idadi hiyo ya nafasi nane ambazo Diarra ameokoa katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika, inamfanya awe na wastani wa kuokoa mashuti 2.7katika kila mchezo.

Katika mechi hizo tatu, Diarra alitoka bila kuruhusu nyavu zake dhidi ya AS FAR na JS Kabylie ambazo zinaonesha kuwa zitamaliza zikiwa chini ya Al Ahly na Yanga katika msimamo wa kundi hilo zitatuowa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrima msimu huu. Uhodari wa Diarra umeifanya Yanga iwe na takwimu bora zaidi za kiulinzi katika mechi tatu za mwanzo za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika kulinganisha na mara tatu tofauti hapo nyuma ilipowahi kushiriki hatua hiyo.

Wakati katika mechi tatu za mwanzo msimu huu ikiwa imeruhusi nyavu zake kutikiswa mara mbili, mwaka 1998 katika idadi hiyo ya mechi, Yanga ilifungwa mabao tisa na katika msimu wa 2023/2024, ilifungwa mabao sita katika mechi tatu za mwanzo kwenye Ligiya Mabingwa. Msimu uliopita, Yanga katika mechi tatu za mwanzo za hatua ya makundi, iliruhusu nyavu zake kutikiswa mara tano. Yanga sasa inahitajika angalau kupata ushindi katika mechi mbili kati ya nne zilizobakia kwenye kundi hilo ili iweze kutinga robo fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *