#HABARI: Huduma ya Kitaifa ya Polisi nchini Kenya (NPS), imeanzisha uchunguzi kuhusu shambulio lililofanyika Jumapili ya Januari 25, 2026 katika Kanisa la St. Peter’s ACK lililopo Witima, Kaunti Ndogo ya Othaya, Nyeri.
Wakati wa tukio hilo la Jumapili, vilipuzi vilirushwa ndani ya Kanisa, hali iliyozua hofu na kusababisha ibada kukatizwa, ambapo miongoni wa walioshiriki ibada hiyo ni aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua pamoja na washirika wake.
Kwa mujibu wa NPS, vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa magari kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya eneo la kanisa, hakuna majeruhi walioripotiwa.
Huduma ya Polisi imelaani shambulio hilo, ikisema kuwa ni halikubaliki kabisa na halina nafasi katika nchi.
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, pia amelaani shambulio hilo, akisema waliohusika watakabiliwa na matokeo ya vitendo vyao.
“Polisi lazima wachukue hatua bila woga wala upendeleo na washughulikie kwa uthabiti wafadhili na waliotekeleza kitendo hiki bila kujali hadhi yao katika jamii au mwelekeo wao wa kisiasa,” Murkomen aliongeza.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.