#HABARI: Zaidi ya wanafunzi 550 wenye uhitaji katika Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wamekabidhiwa vifaa vya kujifunzia vikiwemo madaftari na sare za shule na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega.

Msaada huo unalenga kuwawezesha wanafunzi hao kuendelea na masomo bila kukwama kwa kukosa mahitaji muhimu, huku wanafunzi wakiiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya shule ili wapate elimu bora zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi. Khadija Ali, amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wanapelekwa shule na kusimamiwa vyema ili kutumia fursa hiyo ya elimu kujenga mustakabali wao.

Kwa upande wake, Mhe. Ulega amesisitiza dhamira yake ya kuendelea kusaidia sekta ya elimu jimboni humo, akibainisha kuwa kuwekeza kwa watoto wenye uhitaji ni hatua muhimu katika kuimarisha maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *