
Umoja wa Ulaya unaweza kuamua Alhamisi hii kuongeza Walinzi wa Mapinduzi wa Iran (IRGC) kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi ili kukabiliana na ukandamizaji ” zaidi” katika historia ya hivi karibuni ya Iran, amesema mkuu wa sera za kigeni wa EU Kaja Kallas.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Ukitenda kama gaidi, lazima utendewe hivyo,” amesema mkuu wa sera za kigeni wa EU Kaja Kallas, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri 27 wa mambo ya nje wa EU huko Brussels.
“Natarajia (…) kwamba tutakubaliana kuongeza Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Iran kwenye orodha ya makundi ya kigaidi,” ameongeza.
Sik ya Jumatano Ufaransa ilitangaza kwamba sasa iko tayari kufanya uamuzi wake, na hivyo kuondoa moja ya vikwazo vikuu mara makubaliano yatafikiwa.
“Hakuwezi kuwa na kutokujali kwa uhalifu uliofanywa,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot alipowasili Brussels.
Waziri pia alitoa wito kwa mamlaka ya Iran kuwaachilia wafungwa na “kukomesha mauaji yanayoendeleza ukandamizaji mkali zaidi katika historia ya kisasa ya Iran.”
Mwenzake wa Uhispania, José Manuel Albares, pia amethibitisha kuunga mkono uamuzi wa EU. “Ninaamini ni wajibu wa Umoja wa Ulaya kutumia vyombo vyote tulivyo navyo kukomesha ukandamizaji huu.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Maxime Prévot pia amethibitisha kwamba nchi yake iko tayari kuwafuata washirika wake wa EU, “kwa kuzingatia ukatili” ulioshuhudiwa katika wiki za hivi karibuni.
“Matokeo mabaya” Mrengo wa kiitikadi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unashutumiwa na mashirika ya haki za binadamu kwa kupanga ukandamizaji mbaya wa harakati kubwa ya maandamano inayotikisa nchi, na kusababisha maelfu ya vifo.
Inatarajiwa kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya watapiga kura leo, Alhamisi, Januari 29, kuhusu kuweka vikwazo vipya dhidi ya watu wanaokiuka haki za binadamu na kampuni 10 zinazohusishwa na utengenezaji wa ndege zisizo na rubani (drones) za Iran.