#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa mkandarasi wa Kampuni ya M/s Silo Power aliyepewa jukumu la kusambaza umeme katika vitongoji 214 mkoani humo.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 32.3 unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 7,500 na kukamilika ndani ya miaka mitatu, huku RC James akisisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu na vifaa vya ujenzi ili malengo ya serikali yafikiwe kwa wakati.

RC James amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya nishati, akibainisha kuwa vijiji vyote 360 vya Iringa tayari vina umeme na sasa nguvu inaelekezwa vitongojini.

Amesema mkoa huo una mahitaji makubwa ya nishati kutokana na kuongezeka kwa viwanda vidogo na vya kati, hivyo mradi huu ni fursa adhimu kwa wananchi kuanzisha shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi wao kuanzia ngazi ya vijijini.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amemsisitiza mkandarasi kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa wanaozunguka maeneo ya mradi ili waweze kunufaika kiuchumi.

Kwa upande wake, mwakilishi wa REA amebainisha kuwa hadi sasa vitongoji 1,458 mkoani Iringa tayari vimefikiwa na umeme, huku kampuni ya M/s Silo Power ikiahidi kukamilisha kazi hiyo kwa weledi na kuzingatia maelekezo ya serikali kuhusu ushirikishwaji wa nguvu kazi ya wenyeji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *