
Jeshi la Iran limetoa onyo kali kwamba kitendo chochote kipya cha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kitakabiliwa na jibu kali na la haraka, likisisitiza kwamba uzoefu na tajiriba ya vita vya Juni vimebadilisha kimsingi muelekeo wa kijeshi wa Iran na kanuni zake za makabiliano.
Akizungumza kwenye kipindi cha televisheni cha “Kuelekea Upeo wa Palestina” (To the Horizon of Palestine), msemaji wa Jeshi Brigedia Jenerali Mohammad Akraminia amesema Vikosi vya Ulinzi vya Iran sasa vinafanya kazi chini ya maagizo yaliyokwisha bainishwa wazi ambayo hayatoi fursa ya uchelewaji ikiwa adui atarudia “kufanya makosa ya kimahesabu.”
“Ikiwa adui atachukua hatua nyingine ya kijinga na kufanya makosa ya kimahesabu, tutatoa jibu papo hapo na wakati huo huo” ameelza Akraminia.
Msemaji wa jeshi amekumbusha kuwa, Trump aliitaka Iran isalimu amri wakati wa vita vya siku 12 lakini mara akachukua hatua haraka ya kusimamisha uchokozi baada ya kukabiliwa na nguvu ya uzuiaji hujuma ya Iran.
“Trump alitaka Iran isalimu amri, lakini baada ya siku chache alihangaika kusimamisha vita,” ameeleza msemaji wa jeshi na kuongeza kwamba: “katika vita hivyo, Vikosi vya Ulinzi vilionyesha uwezo wao wa kuzuia hujuma, na tukaulazimisha utawala wa Kizayuni kusitisha vita.”
Ameonya pia dhidi ya kujengeka dhana yoyote huko mpya huko Washington kwamba mara hii litafanywa shambulio dogo tu au la kiishara na kuhitimishwa haraka.
“Hii si sinario ambapo rais wa Marekani ataamuru kufanywa operesheni kisha masaa mawili baadaye atuma ujumbe kwenye Twitter kwamba, “kila kitu kimemalizika,” ameonya msemaji wa jeshi na kusisitiza: “Aina hiyo ya mawazo ni ndoto tu. Shambulio kama hilo lintawasha moto ambao utagubika eneo lote la Asia Magharibi.”
Akraminia ametamka bayana kwamba wigo wa kijiografia wa makabiliano yoyote yajayo hautakuwa na mpaka.
“Wigo wa vita bila shaka yoyote utaenea katika eneo lote,” amesema. “Kuanzia kwenye utawala wa Kizayuni hadi nchi zenye vituo vya kijeshi vya Marekani, zote hizo zitakuwa walengwa wa makombora na ndege zetu zisizo na rubani”…/