Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikaribishi vita, lakini itatoa jibu kali na la haraka kwa uvamizi wowote dhidi yake.

Rais Pezeshkian amesema hayo leo katika mazungumzo ya simu na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan ambapo sambamba kuthamini himaya na misimamo ya nchi za Kiislamu kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa juhudi endelevu na zilizoratibiwa na nchi za kikanda ili kupunguza mivutano na kusaidia kuanzisha amani na utulivu.

Akielezea utendaji wa kimsingi wa Jamhuri ya Kiislamu kuhusu sera za kigeni, Rais wa Iran ameeleza kuwa, kuimarisha na kupanua uhusiano na nchi jirani na za Kiislamu katika nyanja zote ni miongoni mwa vipaumbele vya kimkakati vya taifa hili.

Aidha amesema: Kuimarisha uhusiano wa kindugu, kuimarisha umoja na mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu, na kupanua ushirikiano wa kikanda ni miongoni mwa nguzo za msingi za sera ya kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Pezeshkian ameashiria vitendo vya uadui vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa la Iran, ikiwa ni pamoja na kutumia mashinikizo na vikwazo, vita vya kutiwishwa vita vya siku 12, na uchochezi na uungaji mkono kwa wafanya fujo katika vurugu za hivi karibuni, pamoja na misimamo ya vitisho na vita na kusisitiza kwamba, kudumisha usalama na kuanzisha amani na utulivu wa kudumu katika eneo hili ni miongoni mwa vipaumbele vya msingi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesisitiza kuwa, “Iran haijakaribisha na haitakubali vita kwa njia yoyote ile na haioni vita kuwa kwa maslahi ya upande wowote, hata hivyo, kwa bahati mbaya, pande za Magharibi zimeonyesha kupitia vitendo vyao kwamba, licha ya madai yao, kivitendo hazishikamani na diplomasia wala haziheshimu sheria za kimataifa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *