#HABARI: Sakata la Pombe kuwaathiri wanaume wakiwemo vijana katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wazee katika wilaya hiyo kapaza sauti wakiiomba Serikali kukomesha Pombe zinazotengenezwa na kutumika bila kuthibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Aidha, wananchi hao wamesisitiza kufanyika kwa ufuatiliaji wa kutosha juu ya biashara hizo kwani zinawaathiri vijana kwa kiasi kikubwa na zinachangia kuongeza umasikini usio wa lazima kwa vijana, wazazi, jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao watendaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamethibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo na wamesema hatua zinaendendelea kuchukuliwa ikiwemo ya kutoa elimu kwa jamii japo wamesema ushirikiano zaidi unahitajika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.