#HABARI: Jeshi la Uganda limekiri kuwa wanajeshi walimkamata kwa muda mfupi Barbara “Barbie” Kyagulanyi, mke wa kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine, na baadaye kumuachia huru, huku wakiashiria kuwa alisaidia katika jitihada za kumtafuta mumewe.

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Kiongozi wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Uganda, aliweka picha ya Barbie wakati wanajeshi walipochukua hatua hiyo usiku wa Januari 23 katika eneo la Magere, Wilaya ya Wakiso.

Jenerali Kainerugaba alisema: “Walimkamata na kisha kumuachia huru. Alikuwa msaada mkubwa katika kutupatia taarifa za mumewe.”

Hata hivyo, Jenerali Kainerugaba amekana madai ya kudhalilishwa kwa mke huyo. Ameashiria kuwa jeshi halidhalilishi wanawake na lengo kuu ni kumtafuta Bobi Wine, sio kuwadhalilisha wanafamilia wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *