#HABARI: Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Korea (KOICA), imezindua mpango kabambe wa barabara za kasi (Expressways) unaolenga kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafirishaji nchini.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amebainisha kuwa mpango huu ni sehemu ya mikakati ya kuchochea ukuaji wa uchumi na kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Katika kufanikisha maandalizi ya mpango huo, Serikali ya Korea imetoa ruzuku ya dola za Kimarekani milioni tano kupitia mkataba uliosainiwa Agosti 2025 kati ya Wizara ya Fedha na KOICA.

Meneja wa Miradi ya Ubia (PPP) kutoka TANROADS, Mhandisi Elibariki Mkumbo, ameeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo kwa mwaka huu utasaidia kuweka msingi imara wa ujenzi wa barabara za kisasa zitakazosaidia kukuza biashara na kurahisisha huduma za kijamii kote nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *