#HABARI: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetangaza kuwa itaendesha zoezi la upimaji wa viashiria vya saratani ya tezi dume bila malipo wakati wa tamasha la IST Festival litakalofanyika Februari 14, 2026 katika ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dkt. Mbonea Yonazi, ameema kuwa dhamira ya hospitali ni kuwasogezea wananchi huduma za ubingwa bobezi pale inapopata fursa ya kufanya hivyo na kuongeza kuwa IST Festival ni jukwaa muhimu linaloiwezesha hospitali kukutana moja kwa moja na wananchi na kutoa huduma za afya kwa urahisi zaidi.
Dkt. Mbonea ameeleza kuwa upimaji wa viashiria vya saratani ya tezi dume kwa sasa unatumia njia ya kisasa zaidi inayohusisha uchunguzi wa sampuli ya damu, ambapo majibu hupatikana ndani ya muda mfupi ambapo amebainisha kuwa njia hiyo ni tofauti na ile ya awali iliyokuwa ikitumika na kuzoeleka kwa wananchi wengi.
Aidha, amewahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha hilo, si tu kwa ajili ya kupima afya zao, bali pia kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika sambamba na tukio hilo, kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.