#HABARI: Wizara ya Nishati imewahimiza wananchi wa Wilaya ya Monduli kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake kugeukia nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi, hatua itakayosaidia kulinda mazingira na afya za walaji kutokana na madhara ya moshi na uharibifu wa misitu.

Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Nolasco Mlay, ametoa wito huo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo ya Ofisi ya Makamu wa Rais yanayozitaka taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 100 kutumia nishati safi.

Mlay amesisitiza kuwa mazingira ni ajenda ya kimataifa na ni wajibu wa kila mwananchi kubadili mtazamo kwa kuacha kutafuta kuni na kuanza kutumia nishati salama na za kisasa.

Aidha, Wizara imewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa kusimamia vyema maelekezo ya serikali na kufichua changamoto zinazozikabili taasisi katika mchakato huo wa mabadiliko.

Ushirikiano huo wa viongozi wa ngazi za chini unatajwa kuwa nguzo muhimu inayoiwezesha serikali kufahamu vikwazo vilivyopo na kuchukua hatua stahiki ili kufikia malengo ya kitaifa ya nishati safi kwa manufaa ya jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *